You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo:...

8
You are the Entrepreneurs of tomorrow!

Transcript of You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo:...

Page 1: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

You are theEntrepreneursof tomorrow!

Page 2: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

Tumeshafanya ugunduzi mkubwa wa gesi asilia nchini Tanzania na inasadikika kuwa Tanzania itakuwa kati ya nchi wazalishaji wakubwa wa gesi barani Afrika. Hili linatufanya tuhitaji wajasiriamali wengi wazawa ili kutoa ushirikiano katika sekta hii inayokuwa kwa kasi. Je ungependa kuwa sehemu ya wajasiriamali hao na kutoa mchango wako kwakatika sekta hii kwa kuwa na biashara yako mwenyewe? Shiriki katika shindano letu.

Statoil inakukaribisha kushiriki katika shindano la Mashujaa wa kesho

Stat

oil´s

invo

lvem

ent i

n Ta

nzan

ia. P

hoto

: Hei

ne M

elke

vik

Page 3: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

Statoil ni kampuni ya nishati ya kimataifa yenye kufanya shughuli zake katika nchi 36 duniani kote. Statoil ina uzoefu wa miaka 40 katika masuala ya mafuta na gesi na imejikita katika kuwekeza teknolojia ya hali ya juu kuhakikisha kuwa inatoa suluhisho kwa masuala yote ya nishati duniani. Makao makuu ya Statoil yako nchini Norway na kampuni hii inasadikiwa kuwa na wafanyakazi takribani 20,000 duniani kote. Statoil imesajiliwa katika soko la hisa la New York na Oslo.

Statoil ilianza shughuli zake nchini Tanzania tangu mwaka 2007, iliposaini Mkataba wa Pamoja wa Uzalishaji (PSA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa ajili ya Kitalu Namba 2. Statoil Tanzania AS ndio mwendeshaji anaye shiriki kwa kiwango cha 65% cha hisa na ExxonMobil Exploration and Production Limited kwa kiwango cha uwekezaji cha 35%.TPDC ni wawekezaji wa hisa ya asilimia 10% ya leseni endapo kutathibitika kuwepo kiwango cha gesi cha kuwezesha biashara. Statoil na mshirika wake wamefanya ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kitalu namba 2 eneo linalokadiriwa kuwa na takribani kilomita za mraba 5,500 likiwa kwenye kina cha maji cha urefu wa mita kati ya 1,500 na 3,000. Ugunduzi huu unakadiriwa kuwa 22Tcf (ujazo wa gezi) nahii inapelekea maendeleo makubwa ya mradi wa gesi asilia nchini Tanzania.

Statoil

Statoil nchini Tanzania

Statoil inaamini katika kuwasaidia vijana wenye vipaji katika nchi ambazo tunafanya shughuli zetu za uchimbaji na uenedelezaji wa nishati. Tunaamaini katika kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao. Kwa njia hii tunaamini tunachangia katika kuendeleza jamii zinazotuzunguka.

Statoil inawajali mashujaa wa kesho

Page 4: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

Shindano la Mradi wa Biashara

Vigezo na Masharti ya shindano Washiriki wanaweza shiriki shindano katika vikundi au mtu mmoja mmoja. Kikundi kisizidi watu watatu• Washiriki wawe na umri wa 18 – 25 na ni LAZIMA wawe wanaishi Mtwara au Lindi• Mshiriki/Kikundi cha washiriki kitaruhusiwa kuwasilisha wazo moja tu la biashara• Mshiriki/Washiriki watapaswa kujaza fomu inayopatikana katika kipeperushi hiki• Mshiriki/Washiriki wanaweza kushiriki kwa kutumia lugha ya kiingereza au Kiswahili• Wazo la biashara lazima lilenge mazingira ya Mtwara na liweze fanyika Mtwara pia.• Mshiriki/Washiriki ni lazima walete wazo la biashara au mpango wa biashara walioundaa wenyewe• Tarehe ya mwisho kukusanya wazo la biashara itakuwa ni 20 Desemba, 2015• Mawazo bora ya biashara yatachaguliwa na washiriki watapewa mafunzo ya namna ya kuandika mpango wa biashara • Washiriki wa tano bora watatakiwa kutetea mipango yao ya biashara mbele ya majaji wa shindano hilo.• Mshindi atatangazwa tarehe 14 Aprili, 2016• Mshindi atapata zawadi ya dola 5000 za kimarekani• Washindi wanne watakaofuata watapata zawadi ya dola 1,500 za kimarekani kila mmoja (au kila kikundi)• Mshindi wa shindano atatakiwa kuandika ripoti ya kuonesha jinsi ambavyo fedha alizopata kutoka Statoil zimemsaidia katika kufanya biashara yake. Hili litapaswa kufanyika miezi nane baada ya mshindi kutangazwa.• Wafanyakazi wa Statoil wala ndugu zao wa karibu hawataruhusiwa kushiriki shindano hili

Unaweza tuma wazo lako la kibiashara kwa anuani zifuatazoE-Mail: [email protected] 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)Unaweza pia wasilisha wazo lako katika vituo vifuatavyo;1. Stella Maris University2. Naliendele Agricultural Insititute3. Chuo cha Utumishi wa Umma4. Chuo cha TIA5. Chuo cha VETA6. Pride FM Radio7. Ofisi za Statoil Mtwara Shangani (mbele kidogo ya Maisha Club)8. Maktaba ya Mkoa wa Mtwara

Shindano la mradi wa biashara la Mashujaa wa kesho lilianzishwa mwaka 2014 ili kuwawezesha vijana mkoani Mtwara kujiajiri kwa njia ya ujasiriamali.Tunawatia moyo vijana kushiriki katika shindano hili la mashujaa wa kesho ili waweze kuzitumia fursa mbalimbali zinazoibuka kutokana na uwepo wa shughuli z asekta ya nishati ya gesi asilia mkoani Mtwara. Shindano hili linalenga mawazo ya biashara ndogo ndogo zinazoweza fanyika mkoani Mtwara.

Shindano hili kwa mwaka 2015 litazinduliwa tarehe 27 Novemba. Shindano litakuwa na awamu mbili; kwanza kutoa wazo la biashara ambapo mwisho wa kukusanya mawazo ya biashara utakuwa ni tarehe 20 Desemba, 2015 saa kumi kamili jioni. Mawazo haya ya biashara yatachujwa na mnamo tarehe 20 Januari 2016 mawazo arobaini ya kwanza yatatajwa na wahusika watafahamishwa ili waweze kuanza kushiriki semina ya mafunzo ya namna ya kuandika mpango wa biashara. Mipango ya biashara itakusanywa tarehe 29 Februari na mnamo tarehe 15 March mipango kumi bora ya biashara itatajwa na washindi watakabidhiwa kwa majaji ili kuweza kupata tano bora na hatimaye kumi bora. Mshindi wa shindano la Mashujaa wa Kesho kwa mwaka 2015 atatngazwa tarehe 14 Aprili, 2016.

Page 5: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

Statoil ina mfano halisi wa kuigwa kutoka nchini Norway unaoonesha kwamba nchi inaweza kufaidika kupitia uwepo wa nishati. Uzoefu huu unatuhamasisha tushiriki zaidi katika kuwawezesha wazawa kwa kuboresha vipaji vyao na kuwaonesha fursa zinzaoweza kupatikana kutokana na uwepo wetu kwenye eneo husika. Tungependa faida hii ionekane pia katika jamii ya kitanzania na shindano hili la Mashujaa wa kesho litakuwa sehemu kub-wa ya kutimiza mpango huu

Genevieve Kasanga Meneja Mahusiano, Statoil Tanzania

Page 6: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)
Page 7: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

SEHEMU YA KWANZA:Personal Information/Taarifa binafsiContact person/Jina la mshindani

Date Of Birth/Tarehe ya kuzaliwa:

Phone No/Nambari ya simu

Email address/Barua pepe

FIRST/KWANZA MIDDLE/KATI SURNAME/UKOO

Name team members/Jina la washiriki wa timu

FIRST/KWANZA MIDDLE/KATI SURNAME/UKOO

DAY/SIKU MONTH/MWEZI YEAR/MWAKA

Phone number

SEHEMU YA PILI:Business Application/fomu ya maombi ya biasharaConcept/Dhana/Maelezo ya biashara.Describe your business. What is your business (idea)? What need did you identify in your society? What makes your idea unique? Unafanya biashara gani? Je,unatatua tatizo gani katika jamii yako? Kipi kinafanya biashara yako iwe ya kipekee?

Application form: Heroes of Tomorrow Competition

Page 8: You are the - darecha.orgdarecha.org/wp-content/uploads/2015/12/NEW-Brochure-HOT.pdf · Photo: Heine Melkevik. ... P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)

CO

S 1

40

33

3 P

hoto

fron

t pag

e: O

le Jø

rgen

Bra

tland

I AGREE WITH THE TERMS AND CONDITIONS OF THE COMPETITION.NAKUBALIANA NA ISTILAHI NA MASHARTI YOTE YA SHINDANO.

Personal signature/Sahihi yako:............................................................................................... Date/Tarehe: ......./........./2015

Profit/Faida ya biashara yako:How are you making/ going to make profit? How are you going to use your profit to grow your business?Eleza jinsi unavyotengeneza au utakavyotengeneza faida. Utaitumia vipi faida utakayoipata kuendeleza biashara?

Target market/Soko la biashara yako:Who does your business target? Biashara yako inalenga watu gani ? Kwa nini inalenga watu hao?

The business idea form can be delivered by:Fomu hii yaweza wasilishwa katika mifumo ifuatayo:

E-Mail: [email protected] Mail: Statoil, att: tanzaniahot2015, P.O.Box 713 Dar es Salaam

In Person/ Au unaweza peleka katika kituo chochote kati ya vilivyotajwa hapa chini: 1. Stella Maris University 2. Naliendele Agricultural Insititute 3. Chuo cha Utumishi wa Umma 4. Chuo cha TIA 5. Chuo cha VETA 6. Pride FM Radio 7. Ofisi za Statoil Mtwara Shangani (mbele kidogo ya Maisha Club) 8. Ofisi ya Maktaba Kuu ya Mkoa wa Mtwara Fomu zote zilizojazwa ziwe zimesharudishwa kabla ya saa 8 kamili mchana tarehe 20 Desemba, 2015

www.statoil.com/tanzaniahot2014